MAMLAKA YA HALI YA HEWA NCHINI TMA YATOA TAHADHARI YA MVUA KATIKA MIKOA YA KANDA YA ZIWA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na BMG
Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania TMA, imetahadharisha kuhusu
uwezekano wa kunyesha mvua kubwa itakayoambatana na ngurumo katika mikoa ya
kanda ya ziwa ukiwemo mkoa wa Mwanza.
Taarifa ya utabiri wa mamlaka hiyo inaonesha kuwa mvua hizo
zitanyesha kati ya leo na alhamisi wiki hii na kuwaasa wakazi wa mikoa ya Mara,
Kagera, Mwanza, Simiyu, Geita, Shinyanga na Kigoma kuchukua tahadhari.
Tayari mvua hizo zimeanza kunyesha katika baadhi ya maeneo jijini Mwanza
hali inayoweza kusababisha athari za kimiundombinu hasa barabara kutokana na
mitaro mingi ya maji machafu kujaa takataka na kushindwa kupitisha maji.
Kwa upande wa kiwango cha joto, mamlaka hiyo imebainisha kuwa mkoa
wa Mwanza kiwango cha juu cha joto kitakuwa sentigredi 26 huku kiwango cha
chini kikiwa sentigredi 18.
No comments: