LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC MAKONDA KUTAFUTA SULUHU YA UKOSEFU WA MAJI BAADHI YA MAENEO JIJINI DAR ES SALAAM.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Image result for PAUL MAKONDANa James Salvatory, BMG_Dar
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, leo anatarajiwa kufanya ziara katika maeneo mbalimbali yaliyo na uhaba wa maji katika mkoa wake ili kufanya tathimini ya kuhakikisha maeneo hayo yanapata huduma ya maji.

Makonda aliyabainisha hayo jana wakati akizungumza na wanahabari ambapo alibainisha kwamba miongoni mwa maeneo yenye tatizo la maji atakayoyatembelea ni pamoja na Ubungo na Mbezi.

Alisema kumekuwa na kilio cha siku nyingi juu ya wakazi wa maeneo hayo juu ya upatikanaji wa maji kwa hiyo hivyo ziara yake itafanya tathmini kujua ukubwa watatizo kwa ajili ya ufumbuzi.

Ziara hiyo itaenda sambamba na zoezi la uhamasishaji suala la upandaji miti katika maeneo hayo ambapo mgeni rasmi wazoezi hilo anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais, Mama Samia Hassan.

No comments:

Powered by Blogger.