LIVE STREAM ADS

Header Ads

SERIKALI YAJIPANGA VYEMA KUANDAA MBEGU BORA ZA PAMBA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Image result for zao la pambaNa Judith Ndibalema, Mwanza
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt.Charles Tizeba,  amesema serikali imejipanga kuandaa mashamba ya uzalishaji wa  mbegu bora wa zao la pamba.

Hii ni kutokana na tatizo la upatikanaji wa mbegu bora hasa katika zao la pamba na uhitaji wa mbegu hizo,kwani wazalishaji hawajaweza  kufikia robo  ya mahitaji hayo , mpaka sasa wameweza kuzalisha tani 350 wakati Kanda ya Magharibi inahitaji tani 21000.

Dkt.Tizeba alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na  baadhi ya wadau wa pamba katika  kikao, kilicholenga  kujadili namna ya kufanya maandalizi ya msimu wa kilimo wa zao hilo,ili kujipanga na kutambua mapungufu yaliyopo,kilichofanyika katika ukumbi wa Mwanza hoteli mkoani hapa.

"Serikali bado inafanyia kazi suala la upatakanaji wa mbegu bora,hasa kwa zao la pamba kwani wazalishaji wameshindwa kufikia  robo ya mahitaji katika Kanda ya Magharibi ambayo  inahitaji tani 21000 na mpaka sasa wameweza kuzalisha tani 350,hivyo serikali tumejipanga kuandaa mashamba kwa ajili ya kuzalisha mbegu bora, hili mwakani mkulima apate mbegu hizo kwa urahisi na wakati, " alisema Dkt. Tizeba.

Pia aliiagiza Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania ( TOSCI),  kufikia oktoba 5, iwe imeanza ugawaji wa mbengu za pamba ambazo zipo tayari katika maeneo ambayo msimu wa kilimo unawai kuanza, ikiwemo Biharamulo,Kombe,Geita na chato pamoja na kuhakikisha baada ya wiki tatu wawe wameishapata na kuzifanyia majaribio tani 10000.

Hata hivyo alisema, katika kuendeleza zao hilo serikali imetenga bilioni 5 kwa ajili ya pamba,hivyo kupitia fedha hizo na za Mfuko wa Wakfu wa kuendeleza zao la Pamba( CDTF) watafanya mchakato wa kuwapatia wakulima sawa bure.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Pamba James Shimbe alisema, katika msimu wa kilimo mwaka 2016/2017, wakulima wanatarajia kulima zaidi ya ekari  milioni 1( hekta 400000) kwenye Kanda ya Magharibi pamoja na CDTF kuagiza chupa 500000 za viuatilifu, zenye uwezo wa kuhudumia ekari 166,666 kwa kunyunyuzia mara tatu kwa kila ekari kutokana na uwezo wa kifedha wa mfuko huo kushuka katika msimu huu.

Pia alisema,bodi hiyo ilielekeza makampuni yaliyonunua pamba msimu huu wa ununuzi kuhifadhi jumla ya yani 21000 za mbegu za kupanda,kutoka maeneo ambayo hayana ugonjwa wa mnyauko fuzari,hii ni kutokana na ukosefu wa mbegu bora za kutosha katika kuhakikisha eneo hilo linahudumiwa.

Vilevile alisema, katika msimu huu wa kilimo cha pamba mbegu itakayosambazwa kwa wakulima kiasi kubwa itatokana na mfumo ambao siyo rasmi na kiasi kidogo cha tani 400 cha mbegu bora (UKM08) kutoka Quton.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania John Msemwa alisema, hadi kufikia mwezi semptemba  mwaka huu,walikua wameishachukua sampuli 239 kutoka kwa wachambuzi 13 na kampuni 1, zinazowakilisha tani 138.3 za mbegu zisizo na manyoya na zenye manyoya tani 5836.7, huku upimaji wa sampuli hizo unaendelea na matokeo yanatarajiwa kuwa tayari ifikapo oktoba 5,2016.

Aidha alisema changamoto zinazokumba,mfumo rasmi wa upatikanaji mbegu bora za pamba ni wingi wa wazalishaji mbegu ambao hawana elimu ya uzalishaji,kuwepo kwa wachambuaji wasio tofautisha mbegu za kupanda na za kukamua mafuta pamoja na usambazaji na uhifadhi mbovu usiozingatia kudumisha uhai wa mbegu husika.

No comments:

Powered by Blogger.