LIVE STREAM ADS

Header Ads

ESTHER BULAYA ASHINDA KESI KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU


Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini, Esther Amos Bulaya (Chadema), ameshinda kesi yake ya uchaguzi iliyokuwa ikimkabili, iliyofunguliwa na wanachama wanne wa CCM.

Kesi hiyo ya kupinga matokeo ya uchaguzi ilifunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, lakini ilikuwa inasikilizwa mjini Musoma mkoani Mara.

Wanachama hao walidai uchaguzi uliompa ushindi Bulaya haukuwa huru na haki hivyo kuiomba Mahakama kutengua ushindi wake.

Steven Wassira ndiye alikuwa mgombea wa CCM katika jimbo hilo la Bunda Mjini. Bulaya alishinda kesi ya awali Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza lakini wafungua kesi walikata rufaa Mahakama ya Rufaa ambapo Mahakama hiyo ilitoa maamuzi isikilizwe tena ambapo sasa imefikia tamati. Ilikuwa ikisikilizwa Mjini Musoma mkoani Mwanza.
BMG kwa msaada wa mtandao

No comments:

Powered by Blogger.