LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMPUNI YA NISHATI JUA YAZINDUA KAMPENI YA KUANGAZA AFRIKA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Displaying IMG_20161118_102553.jpgNa James Jalvatory, BMG Dar
Kampuni ya nishati ya jua ya jijini Dar es Salaam inayojulikana kama Paraa Mwanga Limited leo imezindua  kampeni ya Kuangaza Afrika yenye lengo la kuleta mwanga katika nyumba za vijijini kupitia vifaa vyake vyenye ubora wa hali ya juu vya nishati ya jua ikishirikiana na kampuni ya Indian Electronic na kampuni ya USA Electro mechanical.

Kampeni hiyo ambayo iko wazi kwa umma itawezesha familia nyingi kuweza kushinda vifaa vya ubora vinavyotumia nishati ya jua zikiwemo taa za mfumo wa LED, redio za FM, chaja za simu za mkononi na betri, vifaa vya kutengeneza umeme jua (solar panels), televisheni, vingamuzi, majiko ya kutumia gesi

Shindano hili litafanyika kuanzia Novemba 2016 hadi Februari 2017 na linategemewa kufikia vijiji zaidi ya 6,000 katika kampeni hii itakayopita katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Lindi, Mbeya, Iringa, Mwanza na Arusha. Watakaovutiwa kushiriki wanashauriwa kujiandikisha kwa kutuma TZS 500, kwenda kwenye namba ya Airtel money 28668.

Akizungumza katika mkutano na waandishi,  Mkurugenzi mkuu wa Paraa Mwanga bi.kirshnamurthy, amesema anajivunia kuweza kufanya promosheni ya vifaa vya LED na umeme jua katika vijiji vya Tanzania na katika mikoa mingi nchini shughuli za kibishara nyakati za usiku zinakuwa hazipo

"Wanaume na wanawake wanashindwa kutumia muda wao kujiendeleza kiuchumi na watoto wanashindwa kujisomea wakati wa usiku. Vilevile, matumizi ya taa za mafuta ya taa na mishumaa ni gharama na sio salama kwa afya Nishati ya jua ndio suluhisho ya changamoto hizi na kupitia kampeni hii tutapatia nyumba, vijiji, shule na vituo vya afya vilivyopo vijijini fursa ya kuweza kupata vifaa bora kabisa vya nishati jua kutoka India ambavyo wanaweza kuvitumia katika maisha yao yote alisema bi. Krishnamurthy

Droo ya aina ya pili mshindi mmoja atapatiwa zawadi yenye taa za aina ya LED 4, redio ya sola inayotumia remote control na kifaa cha kusomea (flash reader), chaja ya simu na betri. Washindi hawa pia watapata televisheni ya inchi 24 ya aina ya LED, kingamuzi kilichounganishwa mwaka mmoja, jiko la gesi, feni na bima ya afya ya jamii. Kila wiki mshindi mmoja atajipatia zawadi ya draw ya pili.

Pamoja na washindi wa wiki ambao watapatiwa vifaa vya nishati jua, pia makusanyo yatakayopatikana katika kampeni hii yatatumika katika kuweka mwanga katika vijiji vitakavyochaguliwa bure na Kutokana na mafanikio yatakayopatikana katika kampeni hii, asilimia kadhaa ya makusanyo yatapelekwa katika vijiji katika mikoa yenye uhitaji.

No comments:

Powered by Blogger.