LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMPUNI YA RELI NCHINI TRL YAZINDUA HUDUMA MPYA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Displaying IMG_20170331_110817.jpgJames Salvatory, Dar
Kampuni ya reli Tanzania TRL imezindua huduma maalum ya usafirishaji wa shehena ya mizigo  (Block train) kutoka bandari ya Dar es salaam mpaka Bujumbura nchini Burundi.

Akizungumzumza wakati uzinduzi wa ufunguzu wa huduma hiyo kaimu mkurugenzi wa TRL,SHABAN JUMBE KIKO amesema kuwa treni hiyo yenye mabehewa 20 itatumika kubeba mizigo ya wafanyabiashara na watu binafsi ambao watakuwa na shehena kubwa za mizigo kwenda nchini Burundi.

Aidha ameongeza kuwa  treni hiyo itatumika kubeba malighafi za chuma yaan (Iron coils) na itatumia muda wa siku nne kutoka bandari ya Dar es salaam mpaka mjini Bujumbura nchini burundi.
Akizungumzia faida za treni hiyo Kiko amesema kuwa itasaidia kurahisisha shughuli za usafirishaji wa Mizigo baina ya Tanzania na Burundi na nchi jirani zanazopakana na Tanzania kutokana na mizigo kufika kwa wakati na kwa gharama nafuu

No comments:

Powered by Blogger.