LIVE STREAM ADS

Header Ads

WENYE MATATIZO YA MOYO WAZIDI KUPATA MATIBABU NCHINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

 James Salvatory, Dar
Madaktari bingwa sita wa moyo kutoka Hospitali ya Saifee ya mjini Mumbai nchini India pamoja na madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wamefanikiwa kufanya matibabu kwa wagonjwa wenye matatizo ya moyo wapatao 20.

Akizungumza na waandishi wa habari,  jijini Dar es salaam  Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo JKCI Bashir Nyangasa, amesema ujio wa madaktari hao ambayo ilikuwa ahadi ya  Jumuiya ya Mabohora umeokoa zaidi ya milioni 400, ambazo zingetumika kufanya matibabu kwa wagonjwa nane waliofanyiwa upasuaji wa kuvuna mishipa ya damu mguuni na kuipandikiza katika mishipa ya moyo iliyoziba, na upasuaji wa milango miwili hadi mitatu ya moyo ambayo ilikuwa na matatizo.

Aidha amesema kuwa Kwa upande wa upasuaji bila kufungua kifua kwa kutumia mtambo wa Cath Lab wametoa huduma mbalimbali za matibabu ya moyo kwa wagonjwa 12 ambao wamezibua mishipa ya damu ambapo mgonjwa mmoja mshipa wake ulikuwa umeziba kwa asilimia mia na Wagonjwa wote hawa wanaendelea vizuri na wataruhusiwa pindi afya zao zitakapoimarika

Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabohora nchini, Zainuddin Adamje amesema Jumuiya hiyo kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee itaendelea kusaidia matibabu ya wagonjwa wa moyo nchini pamoja na kufadhili madktari bingwa wa moyo kwenda kujifunza katika hospitali hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.