LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAANDISHI WA HABARI ZA KILIMO TANZANIA WAKUTANA JIJINI MWANZA KUPANGA MIKAKATI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Kilimo Tanzania (TAJF), Gerald Kitabu (kulia), akizungumza na waandishi wa habari wanachama wa TAJF wakati wa kikao kilichofanyika Ufukwe wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza juzi ili kujadili masuala mbalimbali ya chama hicho.
 Katibu wa Chama hicho, Elias Msuya akizungumza katika kikao hicho. Kulia ni Mtunza Fedha wa chama hicho, Ellen Manyangu.
 Wanachama wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.

Na Dotto Mwaibale, Mwanza
Waandishi wa Habari wanaounda Chama cha Waandishi wa Habari za Kilimo wamekutana Malaika Beach Resort jijini Mwanza kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ya chama hicho.

Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa chama hicho, Gerald Kitabu pamoja na mambo mengine alihimiza wanachama ambao bado hawajatoa michango yao ya mwaka waitoe ili kutunisha mfuko wa chama hicho.

"Ni muhimu wanachama ambao bado hawajaotoa michango yao kuhakikisha wanaitoa kwa wakati" alisema Kitabu.

Katibu wa Chama hicho, Elias Msuya alisema chama hicho kipo katika mchakato wa kutengeneza vitambulisho kwa ajili ya wanachama na wakati wowote vitakapo kuwa tayari vitatolewa kwa wahusika.

No comments:

Powered by Blogger.