LIVE STREAM ADS

Header Ads

Azam Fc wabwana mbavu ugenini na Mbao Fc

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Judith Ferdinand, Mwanza
Timu ya Mbao FC na Azam FC, jana zimeshindwa kuonyeshana mabavu baada ya kutoka suluhu ya 0-0 katika raundi ya 7 ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/18.

Mbao FC walikuwa wenyeji katika mchezo huo uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, ambapo mpaka dakika 90 zinamalizika hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzie,licha ya mashambulizi kuwa kwa pande zote.

Ikumbikwe kuwa Azam FC imejikuta haifanyi vizuri Kanda ya Ziwa baada ya michezo yote miwili kutoka sare.

Akizungumza mara baada ya mchezo kumalizika Kocha Msaidizi wa Azam FC Iddy Cheche alisema, safari za Kanda ya Ziwa ni hamsini kwa hamsini, kutokana na  wachezaji wa safu ya mbele kuwa chipukizi hivyo wanajipanga katika usajili wa dirisha dogo.

Naye Nahodha wa Azam FC Himid Mao alisema, wako vizuri japo matokeo siyo mazuri kwa kutoka sare  Kanda ya Ziwa  wakati wamezoe kushinda,wanajipanga zaidi katika mchezo ujao , ili waweze kufanya vizuri na kuchukua pointi tatu.

Kwa upande wake Kocha wa Mbao FC Etiene Ndayiragije alisema, matokeo ni mazuri  na uchezaji wa vijana ni mzuri na wanaendelea kuimarika, kwani pointi moja kwao ni nzuri.


Hata hivyo Azam FC tangu kuanza kwa vlp wametoa sare 3 huku Mbao FC wakiwa na 4.

No comments:

Powered by Blogger.