LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ujio wa Rais Magufuli hii leo Jijini Mwanza

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

 Agost 11, 2016 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli, aliweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu la Furahisha Jijini Mwanza. 

Wakati anafanya ziara yake ya siku mbili kuanzia leo Jijini Mwanza, miongoni mwa shughuli atakazofanya ni pamoja na kuzindua daraja hilo ambalo ujenzi wake umekamilika pamoja na kufungua kiwanda cha vinywaji cha Sayona Drinks Limited kilichopo Nyakato na baadaye kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika kwenye uwanja wa Mwatex Nyakato.

Kesho Oktoba 31,2017 Rais Magufuli atafungua kiwanda cha dawa cha Victoria Moulders and Polybagus kilichopo Igogo pamoja na kiwanda cha dawa cha Prince Pharmacetical Industry kilichopo Buhongwa ambapo wananchi wote wanahimizwa kujitokeza kwa wingi kwenye mapokezi ya Rais Magufuli katika maeneo yote atakayopita baada ya kuwasili Jijini Mwanza majira ya saa mbili asubuhi kupitia uwanja wa ndege wa Mwanza.
 Mwonekano wa daraja la watembea kwa miguu, Furahisha Jijini Mwanza.
Rais Dkt.John Magufuli ambapo jana alikuwa akisherehekea kuzaliwa kwake (Alizaliwa Oktoba 29, 1959). Bonyeza HAPA ziara ya Rais Magufuli mkoani Mwanza, mwaka jana.
Binagi Media Group

No comments:

Powered by Blogger.