LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Magufuli azuia bomoa bomoa Jijini Mwanza

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.


Na Binagi Media Group
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli amewasili hii leo Jijini Mwanza, kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.

Baada ya Rais Magufuli kulakiwa uwanja wa ndege wa Mwanza majira ya saa 3:20 asubuhi, alizindua daraja la juu la watembea kwa miguu la Furahisha na baadaye ataelekea kwenye uzinduzi wa kiwanda cha vinywaji cha Sayona kilichopo Nyakato.

Akizungumza kwenye daraja la Furahisha, Rais Magufuli amesitisha zoezi la ubomoaji wa makazi ya wananchi katika eneo la Muhonze wanaodaiwa kuwa kwenye eneo la uwanja wa ndege pamoja na Kigoto wanaodaiwa kuwa kwenye eneo la polisi hadi pale mwafaka zaidi utakapopatikana.

Ujenzi wa daraja la Furahisha uliwekewa jiwe la msingi 10.08.2016 ambapo ujenzi huo umegharibu Bilioni nne.
Rais Dkt.John Magufuli akiwasili uwanja wa ndege wa Mwanza na kulakiwa na mwenyeji wake, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Daraja la Furahisha Jijini Mwanza, ambalo limezinduliwa leo
Rais Magufuli (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Marawa (kushoto).
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella akitoa salamu zake kwenye uzinduzi wa daraja la Furahisha
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akitoa salamu zake kwenye uzinduzi wa daraja la Furahisha
Rais Magufuli akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Jijini Mwanza
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Joseph Nyamhanga akitoa salamu zake kwenye uzinduzi wa daraja la Furahisha
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu akitoa salamu zake kwenye uzinduzi wa daraja la Furahisha
Mbunge wa jimbo la Liwale mkoani Lindi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu akitoa salamu zake akitoa kwenye uzinduzi wa daraja la Furahisha
Mtendaji Mkuu Wakala wa barabara nchini Tanroad, Mhandisi Patrick Mfugale, akitoa salamu zake kwenye uzinduzi wa daraja la Furahisha
Rais Magufuli (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella (kulia)
Rais Magufuli akizungumza kwenye uzinduzi wa daraja la Furahisha Jijini Mwanza
Ujenzi wa daraja la Furahisha uliwekewa jiwe la msingi 10.08.2016 ambapo ujenzi huo umegharibu Bilioni nne.

No comments:

Powered by Blogger.