LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ziara ya Rais Magufuli mkoani Mwanza

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Judith Ferdinand, Mwanza
Rais John Magufuli anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili  mkoani Mwanza, ambapo atazindua   daraja la waenda kwa miguu la Furahisha pamoja na viwanda vitatu.

Akizungumza juu ya ujio huo na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella  alisema,  Rais atawasili oktoba 30  ambapo  atazindua daraja hilo pamoja na kiwanda cha Sayona Drinks Limited kilichopo Nyakato.

Aidha alisema, atahitimisha okotoba 31 kwa kufungua kiwanda cha Victoria Moulders/Polybags kilichopo Igogo pamoja na kiwanda cha dawa cha Prince Pharmaceutical Industry kilichopo Buhongwa ambacho ni kiwanda cha  kwanza kuwa mkoani tofauti na Dar es salaam.
Hivyo aliwataka wananchi na wadau kushiriki kumpokea na watambue kuwa taifa letu ni tulivu na salama na miundombinu kuboreshwa ni njia ya kuleta unafuu kwa wananchi na ufunguzi wa viwanda hivyo ni njia moja ya kutoa ajira na kuongeza pato la serikali.

“Ikumbwe kuwa ni juhudi zake binafsi katika kuboresha miundombinu , kufungua daraja na viwanda  yote ni kudhibitisha kauli mbiu ya Tanzani ya viwanda” alisema Mongella.

Sambamba na hilo aliwataka wanamwanza kutunza miundombinu ili kuleta ufanisi katika shughuli binafsi, za jamii, mkoa na taifa kwa ujumla kwani miundombinu ndio msingi wa maendeleo ya uchumi.

No comments:

Powered by Blogger.