LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wizara ya Mifugo na Uvuvi yatwaa kufuri la dhahabu kwa kubana taarifa

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Mweka hazina wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Jangwa la Sahara MISA tawi la Tanzania Bw. Michael Gwimile akizindua rasmi ripoti ya utafiti wa upatikanaji wa taarifa katika ofisi mbalimbali za umma nchini Tanzania, katikati ni Mama Rose Haji Mwalimu ambaye ni Mwanachama wa taasisi hiyo na Mshauri wa Mambo ya Habari. Hafla hiyo ilifanyika jana katika Hoteli ya Double View jijini Dar es Salaam.
Mweka hazina wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Jangwa la Sahara MISA tawi la Tanzania  Bw. Michael Gwimile (kushoto) na Mama Rose Haji Mwalimu ambaye ni Mwanachama wa taasisi hiyo na Mshauri wa Mambo ya Habari, wakionesha ripoti hiyo baada ya uzinduzi.
Mama Rose Haji Mwalimu ambaye ni Mwanachama wa Taasisi ya MISA Tanzania na Mshauri wa Mambo ya Habari.akisoma taarifa kwa niaba ya Mwenyekiti wa MISA Tanzania Bi.Salome Kitomari juu ya Siku ya kupata taarifa Duniani.
Mama Rose Haji Mwalimu ambaye ni Mwanachama wa Taasisi ya MISA Tanzania na Mshauri wa Mambo ya Habari (Kulia), akitangaza taasisi iliyochukua Tuzo ya Ufunguo wa Dhahabu kwa kufunguka sana kwa umma kwa mwaka 2018 kuwa ni Mfuko wa Hifadhi kwa Watumishi wa Umma (PSPF) . Kushoto ni Mweka hazina  wa  MISA Tanzania  Bw. Michael Gwimile
Mama Rose Haji Mwalimu ambaye ni Mwanachama wa Taasisi ya MISA Tanzania na Mshauri wa Mambo ya Habari (Kulia), akitangaza taasisi iliyochukua Tuzo ya Kufuri la Dhahabu kwa kubana  taarifa kwa mwaka 2018 kuwa ni Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Mweka hazina wa  MISA Tanzania  Bw. Michael Gwimile, akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 28.09.2018. Imeandaliwa na Fredy Njenje.
SOMA>>>TRA WAIBUKA VINARA WA UTOAJI TAARIFA KWA UMMA MWAKA 2016

No comments:

Powered by Blogger.