Wanahabari Mwanza watakiwa kuandika habari na makala kuhusu malezi bora ya watoto
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Matangazo.
Judith Ferdinand, Mwanza
Wanahabari
mkoani Mwanza wametakiwa kuandika habari za kuelimisha jamii kuhusu masuala ya
watoto hususani malezi bora.
Hii ni baada
ya kuonekana kuwa changamoto kubwa inayowakabili watoto na kupelekea kukosa
haki zao katika Mkoa wa Mwanza ni kutokana na
wazazi kukosa elimu na kutokuwa na uelewa kuhusu malezi bora (chanya).
Wito huo
umetolewa na Mratibu wa Utetezi na
Ushawishi wa Haki za Watoto wa Shirika la SOS Children Village's Tanzania, Mpelly Kalonge katika semina ya wadau kuhusu
majadiliano ya utekelezaji wa sera, mipango na mikakati
inayohusu mtoto ili kuwalinda watoto dhidi ya ukatili iliyowakutanisha jumla ya
wadau 28 kutoka Kata sita ambazo mradi wa kuimarisha familia unafanya kazi
ikiwemo Igogo, Mkuyuni, Pamba, Mhandu, Mahina na Bugongwa.
Kalonge
alisema, kupitia semina hiyo wadau walisema changamoto kubwa inayowakabili
watoto ni ukosefu wa elimu na malezi bora kutoka kwa wazazi hivyo ushawishi na
uteteze wa haki za watoto ni jambo linalohitajika, hivyo ili jamii iweze kupata
elimu ya malezi vyombo vya habari vinatakiwa kuandika na kuhabarisha habari
zinazohusu watoto ikiwemo malezo chanya yanayotakiwa kwani kupitia wao ni
rahisi kufikia watu wengi na kwa wakati mmoja.
No comments: