LIVE STREAM ADS

Header Ads

Boss Lady wa Lake FM Mwanza aja kivingine tena

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mbunifu wa Mavazi na Mkurugenzi wa Kituo Cha Redio cha 102.5 Lake FM cha Jijini Mwanza, Doreen Peter Noni akiwa katika pozi.
Mbunifu wa Mavazi na Mkurugenzi wa Kituo Cha Redio cha 102.5 Lake FM Mwanza, Doreen Peter Noni (kushoto), akirekodi kipindi cha Tena na Tena na msanii Vanessa Mdee.
Mbunifu wa Mavazi na Mkurugenzi wa Kituo Cha Redio cha 102.5 Lake FM, Doreen Peter Noni (kushoto) akirekodi kipindi cha Tena na Tena na wasanii Nevi Kenzo.

Mwandishi Maalum
Mbunifu wa mavazi nchini, Doreen Peter Noni anayetamba na lebo ya Eskado Bird ameibuka na kipindi maalum cha televisheni kijulikanyo kwa jina la "Tena Na Tena" ambacho kinazungumzia shughuli mbalimbali za kutafuta riziki katika maisha mpaka kufanikiwa.

Doreen ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu, Mwanzilishi na Mmiliki wa kituo cha redio cha 102.5 Lake FM Mwanza anasema sababu kubwa ya kuanzisha kipindi hicho ambacho kitarushwa katika moja ya vituo vya televisheni hapa nchini, ni kutoa hamasa kwa vijana kuendelea "kupambana" katika kutafuta riziki bila kukata tamaa.

Anasema kipindi cha Tena na Tena ambacho pia kitaonyeshwa "Online", kimerekodiwa kwenye gari inayotembea ambapo muhusika atatoa ushuhuda wake wa maisha katika mfumo wa majadiliano. Alisema kuwa mbali ya kuburudisha, lengo lingine la kipindi cha Tena na Tena ambacho kitaanza kurushwa hewani hivi karibuni ni kutoa elimu kwa vijana katika kukabiliana na changamoto za maisha.

Doreen anasema kuna vijana wengi wanakata tamaa katika maisha bila kujua walikosea wapi, jambo ambalo limemfanya kuandaa kipindi hicho ili kutumika kama nyenzo ya mafanikio. "Wahusika katika kipindi hiki watapata fursa ya kuzungumzia jinsi alivyohangaika mpaka kupata mafanikio. Ni kumbukumbu ambazo haziwezi kusaulika na kutumiwa na waangaliaji wa kipindi hicho kama nyenzo kwa mafanikio ya vijana wa sasa". Anabainisha Doreen.

Katika kipindi hicho, kutakuwa na nafasi ya kutoa burudani kama kuimba kwa mtindo wa karaoke, hali ambayo inamfanya mtazamaji kutochoka kuangalia. Kwa mujibu wa Doreen, mbali ya wajasiriamali, kipindi cha Tena na Tena pia kitafanya mahojiano na watu mbalimbali maarufu, wanasiasa, wanamichezo kwa lengo la kuhamasisha vijana kutokata tamaa katika shughuli za kujitafutia kipato. Unaweza kupata taarifa zaidi katika mitandao ya kijamii ya Tena na Tena kupitia @tenanatenashow facebook, instagram, twitter na youtube.


No comments:

Powered by Blogger.