LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbunge Nyamagana akagua miradi mbalimbali ya maendeleo “vyoo vinatisha”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mbunge Jimbo la Nyamaganamkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM) ameendelea na ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo hilo ikiwemo elimu, afya, maji na barabara kusaidia ukamilishaji wa miradi hiyo kupitia fedha za mfuko wa jimbo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Ziara ya mbunge Stanslaus Mabula pia ilifika katika Shule ya Msingi Amani Kata ya Butimba na kujionea hali tete ya vyoo na kuchangia ukarabati wake.
Mbunge Stanslaus Mabula alifika katika Shule ya Msingi Amani iliyopo Kata ya Butimba na kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha jengo hili kwa ajili ya kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa.
Mbunge Stanslaus Mabula pia aliwasili katika Shule ya Msingi Igoma C na kusaidia ukarabati wa shule hiyo.
Ukarabati ukiendelea katika Shule ya Msingi Igoma C Jijini Mwanza.
Ukarabatai katika Shule ya Msingi Igoma C.
Mbunge Stanslaus Mabula pia alisaidia ujenzi wa Kituo cha Polisi Kata ya Kishiri.
Kituo cha Polisi Kata ya Kishiri Jijini Mwanza.
Mbunge Stanslaus Mabula pia alisaidia ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mahina Kati Kata ya Mahina inayojengwa kwa nguvu za wananchi.
Mbunge Stanslaus Mabula akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali katika Kata ya Mahina.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.