LIVE STREAM ADS

Header Ads

Naibu Katibu Mkuu UWT Taifa "kuweni na amani, Rais Magufuli anawahakikishia ulinzi"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT Tanzania Bara) kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jesca Mbogo ameendelea na ziara yake mkoani Kilimanjaro ambapo pamoja na mambo mengine amewatembelea wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Shule ya Msingi ya bweni Mwereni iliyopo wilayani Moshi na kuwahimiza kusoma kwa bidii kwani Serikali inawahakikishia ulinzi wao.
BMG Habari
Katika ziara hiyo, pia Mbogo aliwakabidhi wanafunzi hao mahitaji mbalimbali ikiwemo mahindi, mafuta ya kupikia pamoja na sabuni.
Naibu Katibu Mkuu UWT Tanzania Bara, Jesca Mbogo akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Mwereni wilayani Moshi.
Mmoja wa wanafunzi wenye mahitaji maalum anayesoma katika shule ya msingi Mwereni wilayani Moshi.
Mahitaji mbalimbali yaliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu UWT Tanzania Bara, Jesca Mbogo katika shule ya Msingi Mwereni wilayaniu Moshi.
Wanafunzi katika shule ya msingi Mwereni wilayani Moshi, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu UWT Tanzania Bara, Jesca Mbogo alipowatembelea shuleni hapo.

No comments:

Powered by Blogger.