LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wavuvi na wachimbaji wadogo wa madini wapewa siku nne kuwa na vitambulisho

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com 

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela akitoa maelezo kuhusu vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo kwa wachimbaji wadogo wa madini katika Kijiji cha Saza Wilayani Songwe
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela akimpatia kitambulisho cha wajasiriamali wadogo wadogo mchimbaji mdogo wa madini katika Kijiji cha Saza Wilayani Songwe.
Afisa Kodi Kutoka Mamlaka ya Mapato nchini TRA Omary Iddi akitoa maelezo kuhusu vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo kwa wachimbaji wadogo wa madini katika Kijiji cha Saza Wilayani Songwe.
Baadhi ya wajasiriamali wadogo wadogo wakipata maelezo na wengine wakichukua vitambulisho vya wajasiriamali katika eneo la Mkwajuni Wilayani Songwe.

SongweRS
Wavuvi na wachimba madini wadogowadogo wamepewa muda wa siku nane kuchukua vitambulisho vitakavyo wawezesha kutambulika rasmi kama wajasiriamali wadogo wadogo ili waweze kufanya shughuli halali za uzalishaji mali bila kusumbuliwa.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela ametoa maelekezo hayo mapema wiki hii akiwa ziarani Wilayani Songwe ambapo ametembelea kambi ya wachimbaji wadogo wa madini katika Kijiji cha Saza na wajasiriamali wa uvuvi katika kambi ya sabasaba pembezoni mwa mto Rukwa.

Brig. Jen. (Mst) Mwangela amesema, “mjasiriamali mdogomdogo unayefanya shughuli yeyote halali inayokuingizia kipato na hulipi kodi TRA serikali inataka kukutambua hivyo basi unatakiwa kuchukua kitambulisho ili usisumbuliwe”.

Aidha amezitaka halmashauri za Mkoa wa Songwe kuhakikisha zinasimamia vizuri ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali wadogo ili kuepuka udanganyifu na kuhakikisha kila mjasirimali anatambulika kwa kupata kitamblisho hicho.

Naye Afisa Kodi Kutoka Mamlaka ya Mapato nchini TRA Omary Iddi amesema wajasiriamali wadogowadogo ambao kipato chao kwa siku wanapata chini ya shilingi milioni nne kwa mwaka wanapaswa kuchukua kiambulisho cha Ujasiriamali ili nao waweze kuchang pato la taifa.

Wajasiriamali wadogo wanaoishi kwenye kambi ya uvuvi ya Sabasaba, Wachimbaji wadogo wa madini wa Saza na wajasiriamali wegine Wilayani Songwe wamezipongeza juhudi za serikali za kuweka mazingira mazuri ya ulipaji kodi kwa manufaa ya maendeleo ya Taifa.

Simkonda Maiko amesema anaipongeza serikali kwa kuwatambua wajasiriamali wadogo wadogo na hivyo kuwawekea utaratibu mzuri wa kuchangia mapato pia itawasaidia kutosumbuliwa.

No comments:

Powered by Blogger.