LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mongella awafuata wananchi walipo kusikiliza na kutatua kero zao

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amejiwekea utaratibu wa kusikiliza malalamiko na kero mbalimbali kwa kukutana na mwananchi mmoja mmoja ofisini kwake kila jumanne.

Kwa wananchi walio nje ya Jiji la Mwanza na ambao wakati mwingine mazingira huwawia vigumu kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mongella amekuwa akiwafuata katika Kata zao ili kuwasikiliza.

Jumanne Machi 12, 2019 baada ya Mongella kuwasikiliza wananchi mbalimbali ofisini kwake, mchana akiwa ameambatana na Watendaji mbalimbali alifunga safari hadi Kata ya Bugogwa wilayani Ilemela na kukutana na wananchi kupitia mkutano wa hadhara ambapo aliwasikiliza kero zao na kuzitolea ufafanuzi/ maelekezo.

Masuala mbalimbali yalielezwa kwenye mkutano huo ikiwemo kero ya upatikanaji wa maji, huduma za afya, upanuzi wa mtandao wa umeme, miundombinu pamoja na ulinzi na usalama ambapo Mongella alitoa maelekezo kwa baadhi ya masuala hayo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza na wakazi wa Kata ya Bugogwa na maeneo jirani kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Bugogwa/ Igombe.
Mkuu wa Mkoa Mwanza aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa Mwanza, Mkuu wa Wilaya Ilemela pamoja na Watendaji mbalimbali
Mmoja wa wakazi wa Bugogwa akieleza kilio chao kuhusu suala la maji ambapo alisema mradi wa maji Bugogwa umechelewa kukamilika na hivyo kuwa kero kubwa kwa wananchi kupata maji safi na salama.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.