LIVE STREAM ADS

Header Ads

Jukwaa la "NAWEZA" latambulishwa Jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mtoa mada, Frank Rweikiza kutoka mradi wa USAID TULONGE AFYA akitambulisha jukwaa la NAWEZA kwa wadau wa afya kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa hii leo Machi 06, 2019. Jukwaa hilo linalenga kuhamasisha utoaji wa huduma za afya ya uzazi na kupunguza vifo vya akinana mama wajawazito kabla na baada ya kujifungua pamoja na watoto chini ya miaka mitano.
BMG Habari
Utekelezaji wa mradi wa USAID Tulonge Afya ulianza Aprili 2017 na utafikia tamati Aprili 2022 ukijitika kutumia majukwaa ya Naweza na Sitetereki katika kuelimisha wananchi kupata huduma za bora za afya ya uzazi.
Mwezeshaji Martha Shakinyau kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akiwasilisha mada kuhudu vifo vitokanavyo na uzazi wa mpango pamoja na watoto chini ya umri wa miaka mitano nchini Tanzania ambapo amesema akinana 556 kati ya 100,000 hufariki kwa mwaka kutokana na uzazi.
Mmoja wa washiriki wa warsha hii, Jamson Michael kutoka Gazeti Mwananchi akiuliza swali.
Washiriki mbalimbali wakiuliza maswali kwenye warsha hii.
Wadau wakifuatilia kwa umakini warsha hii.
Pia vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii vitatumika kufikisha elimu kwa jamii ili kuzingatia umuhimu wa afya ya uzazi.
Viongozi mbalimbali wakiwemo Waganga Wakuu kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mwanza, Mara, Geita, Kigoma na Kagera wameshiriki warsha hii.
Wadau wa afya wakifuatilia warsha hii.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.