LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbunge Viti Maalum atumia Milioni 144.5 kuunga mkono juhudi za maendeleo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na Ofisi ya Siasa na Uenezi, CCM Mkoa Njombe
Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Njombe, Neema Mgaya amesema atika kipindi cha kuanzia Mwezi Janury 2016 hadi Disemba 2018 ametumia kiasi cha Shilingi Milioni 144.5 katika kuunga mkono shughuli mbalimbali za maendeleo mkoani humo.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa kazi zake kwenye Baraza la Umoja wa Wanawake (UWT) mkoani Njombe, Mgaya alisema pesa hizo zimetumika kununua vifaa mbalimbali alivyo vitoa katika sekta tofauti ikiwemo mifuko ya saruji, masuka kwa ajili ya kuboresha huduma kwenye baadhi ya Zahanati na Vituo vya Afya mkoani humo.

Pia alisema amefanikiwa kutoa vyereheni 370 katika vikundi vya akina mama katika Tarafa mbalimbali za Wilaya zote nne za Mkoa Njombe ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuelekea Tanzania ya Viwanda.

"Kuanzia mwezi January 2016 hadi Disemba 2018 nimefanikiwa kutumia kiasi cha Milioni 144.5 kutoka kwenye mfuko wangu binafsi ambapo nimenunua vifaa mbalimbali ikiwemo saruji, mashuka, pamoja na kutoa vyerehani kwenye vikundi vya akina mama vilivyopo katika wilaya zote za Mkoa Njombe". Alisema Mgaya.

Ili kuboresha sekta ya elimu mkoani Njombe, mbunge huyo ametoa vitabu vya masomo ya ziada kwa shule zote za Sekondari za serikali zilizopo mkoani humo pamoja na Shule mbili za Sekondari zilizopo wilayani Ludewa ambazo zipo chini ya Idara ya Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mgaya ameahidi ushirikiano zaidi kwa viongozi wa CCM, Serikali pamoja na wananchi mkoani Njombe kwa lengo la kuchochea maendeleo kwani ni ngumu kufanikiwa bila kuwa na umoja na mshikamano katika utendaji wa kazi.

Naye Anjela Milembe ambaye ni Katibu wa CCM, Idara ya Wanawake (UWT) mkoni Njombe alimpongeza mbunge Mgaya kwa juhudi zake katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo bila kujali itikadi zozote. 
Tazama>>> Mbunge Neema Mgaya asaidia uboreshaji huduma za afya Njombe
Tazama>>> Mbunge Viti Maalum Mkoa Njombe apongezwa kwa juhudi zake
#PamojaDaimaBMG

No comments:

Powered by Blogger.