Wafanyakazi wa Zantel washiriki usafi masoko ya Zanzibar na Dar
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com


Wafanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya Zantel wameshiriki katika zoezi la usafi katika masoko ya kuuza mazao ya Ilala jijini Dar es Salaam na Saateni Zanzibar na kutoa msaada wa vifaa vya kufanyia usafi kwa uongozi wa masoko hayo ikiwa ni moja ya mkakati wa kampuni hiyo kuwajibika na kujitoa kwa jamii.
Na Cathbert Kajuna
Na Cathbert Kajuna

Kupitia zoezi hili Zantel, ina lengo la kuhamasisha wananchi kuwa na utamaduni wa kusafisha maeneo wanayofanyia biashara, kuhifadhi mazingira pamoja na kuelimisha jamii kuhusu madhara ya uchafu na takataka kiujumla.

Mbali na kufanya usafi wafanyabiashara wa katika masoko hayo na wananchi wanaoishi jirani na maeneo hayo walipata fursa ya kuzifahamu huduma zinazotolewa na Zantel ikiwemo huduma ya fedha kupitia mtandao wake ya EzyPesa ambayo inarahisisha maisha kutuma na kupokea fedha sambamba na kufanya mihamala ya malipo ya huduma mbalimbali.


Mkuu wa Mauzo wa Zantel Tanzania Kanda ya Dar na Pwani, Emmanuel Joshua (kulia) akimkabidhi Meneja wa Soko la Ilala jijini Dar es Salaam, Selemani Mfinanga vifaa vya kufanyia usafi wakati wafanyakazi wa Zantel Tanzania walipokwenda kufanya usafi katika maeneo ya soko hilo.
No comments: