LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kama ni mbunge, Bukombe wamempata, anasema na kutenda

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita ambaye pia ni Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mkange, Kata ya Bugelema jimbo humo, baada ya kufanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, jana Machi 02, 2019.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Doto Biteko akicheza ngoma ya asili na jeshi la sungusungu katika Kijiji cha Mkange jimboni humo.
 Mhandisi Joel Nyanda (wa pili kulia) kutoka Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini TARURA Wilaya Bukombe akifafanua jambo baada ya mbunge Doto Biteko kutembelea daraja la Masumbwe linalounganisha wilaya za Bukombe na Mbogwe lililokatika.
 Sehemu ya daraja la Masumbwe linalounganisha wilaya za Bukombe na Mbogwe mkoani Geita.
 Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa kwa nguvu za wananchi katika shule ya msingi Mtakuja ambapo mbunge Doto Biteko aliwaunga mkono kwa kuchangia shilingi Milioni mbili taslimu.
 Mbunge Doto Biteko (kushoto) akitoka kukagua miundombinu ya vyoo katika shule ya msingi ya Kijiji cha Mtakuja Kata ya Bugelenga wilayani Bukombe.
 Mbunge Doto Biteko (kushoto), akimkabidhi diwani wa Kata ya Bugelenga, Baraka Maganga (kulia), shilingi milioni mbili taslimu kuchangia ukamilishaji wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi ya Kijiji cha Mtakuja.
 "mpunga kwa ajili ya maendeleo"
 Mbunge Doto Biteko pia alipita kujionea miundombinu ya Zahanati ya Kijiji cha Bufanka jimboni humo.
Mbunge Doto Biteko akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mtakuja.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko amewapongeza wakazi wa jimbo hilo kwa juhudi zao za kushiriki kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuahidi kuendelea kuwaunga mkono ili kukamilisha miradi hiyo.

Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini alitoa pongezi hizo jana wakati akizungumza kwa nyakati tofauti, kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo afya na elimu iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi.

Akiwa katika Kata ya Bugelenga, Biteko alichangia shilingi milioni mbili taslimu kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na ofisi ya waalimu katika shule ya msingi ya Kijiji cha Mkange. Pia alitoa kiasi kama hicho katika shule ya msingi Mtakuja ili kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Biteko pia alitoa ahadi ya vitanda kwa ajili ya Zahanati ya Kijiji cha Msasani ambayo kwa muda mrefu haijaanza kutoa huduma kwa wananchi na kuhimiza maboresho yanayoendelea katika Zahanati hiyo yakamilike ili ianze kufanya kazi.

Aidha Biteko alitembelea pia daraja la Masumbwe linalounganisha wilaya ya Bukombe na Mbogwe na kujionea uharibifu kwenye daraja hilo ambapo Mhandisi Joel Nyanda kutoka Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini TARURA wilayani Bukombe, aliahidi kulifanyia ukarabati daraja hilo pamoja na barabara ya Mwalo-Iyogelo-Bugelenga-Masumbwe.

Awali Biteko alipokelewa kwa shangwe na wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi katika Kijiji cha Mwalo Kata ya Ushirombo, waliompeleka kujionea ujenzi wa ofisi ya chama hicho ambapo alichangia aliwaunga mkono kwa kutoa shilingi laki tano taslimu.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.