LIVE STREAM ADS

Header Ads

"Unapomnadanganya Waziri Mkuu, unajichimbia kaburi"- DC Kwimba

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wakazi wa Kijiji cha Sangu, Kata ya Mhande wakimsikiliza Mkuu wao wa Wilaya Kwimba mkoani Mwanza, Senyi Ngaga alipofanya ziara ya kuhamasisha shughuli za maendeleo, kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero zao ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika Kata zote 30 za Wilaya hiyo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Kwimba, Senyi Ngaga (katikati) akizungumza na wakazi wa Kata ya Mhande wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya Kwimba, Senyi Ngaga aliwahimiza wakazi wa Kata ya Mhande pia kujikita kulima mazao ya muda mfupi na mrefu yanayovumilia ukame ikiwemo mihogo, mtama, viazi na mahindi ili kujikimu na chakula cha kutosha licha ya kwamba zao lao kuu ni pamba.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kwimba, Pendo Malebeja akizungumza kwenye mkutano baina ya Mkuu wa Wilaya Kwimba na wakazi wa Kata ya Mhande.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kwimba, Pendo Malebeja aliahidi kushughulikiwa kwa kero za wakazi wa Kata ya Mhande ambazo ni pamoja na maji, miundombinu ya barabara pamoja na ununuzi wa pamba mbegu ambayo tayari wameanza kuikusanya katika vituo mbalimbali vya ununuzi.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.