LIVE STREAM ADS

Header Ads

Makanisa ya Kipentekoste Shinyanga yashiriki mazoezi na kuchangia damu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com 
Na Marco Maduhu, Malunde 1 Blog
Umoja wa makanisa ya kipentekoste mkoani Shinyanga umefanya mazoezi ya viungo na mwili pamoja na kuchangia damu ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano za kuimarisha huduma za afya kwa wananchi hususani kuokoa maisha ya mama na mtoto dhidi ya vifo vitokanavyo na uzazi kutokana na kupoteza damu nyingi.

Hayo yamejiri leo Juni 15, 2019 kwenye uwanja wa wamichezo wa Sabasaba na kuongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko ambayo shughuli imeanza kwa matembezi na kukimbia kwa kuzunguka Mji wa Shinyanga na kuhitimishwa kwa kuchangia damu. 

Mwenyekiti wa umoja huo, Askofu Elias Madoshi alisema wao kama viongozi wa kidini wameona ni vyema kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi pamoja na kuchangia damu. 

Alisema juhudi za serikali ya awamu ya tano zinapaswa kuungwa mkono ambapo wananchi wakiwa na afya mgogoro kamwe hawataweza kufaya shughuli za uzalishaji mali na hatimaye nchi kushindwa kukua kimaendeleo na kufikia kwenye uchumi wa kati. 

"Sisi umoja wa makanisa ya kipentekoste mkoani Shinyanga (CPCT) kwa kushirikiana na umoja wa makanisa ya kiinjili (CC) tumeamua kuungana na Serikali kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi ili wawe na afya imara pamoja na kuchagia damu salama ili kuokoa vifo vya mama na mtoto vikonavyo na uzazi kwa kumwaga damu nyingi wakati wa kujifungua" alisema Askofu Madoshi na kuongeza;

"Hivyo tunatoa wito kwa wananchi mkoani Shinyanga wajikite kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao pamoja na kujitoa kuchangia damu salama ambayo itaokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu ikiwamo na kumaliza vifo vya uzazi vitokanavyo na umwagaji damu nyingi" Alihimiza Askofu Madoshi.

Naye mkuu wa Wilaya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Zainab Telack alipongeza umoja hu  kwa kutoa hamasa ya wananchi kushiriki kufanya mazoezi pamoja na uchagiaji wa damu salama.

Alisema mazoezi hayo yalizinduliwa na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan ambapo hufanyika kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi na kuwasihi watumishi wa Serikali kuwa mfano wa kuigwa kushiriki kwenye mazoezi hayo na siyo kuwa wategeaji ambapo ataanza kuwa anapitisha daftari la ukaguzi wa majina ya watumishi wanaoshiriki mazoezi hayo.

Kwa upande wake mratibu wa Damu Dalama kutoka Benki ya Damu Salama mkoani Shinyanga, Dkt. Joel Mdale pia alitoa shukrani kwa umoja huo kwa hamasa hiyo ya uchangiaji wa damu jambo ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uhaba wa damu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Shinyanga na hatimaye kuokoa vifo vya wagonjwa wenye uhitaji wa damu wakiwemo akina mama wajawazito. 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza kwenye shughuli hiyo. Mwenyekiti wa Makanisa ya kipentekoste mkoani Shinyanga, Askofu Elias Madoshi akieleza sababu za kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi na kuchangia damu. Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (katikati mwenye kofia) akiongoza akiongoza wananchi na waumini wa makanisa ya kipentekoste kufanya mazoezi. Mazoezi yakiendelea. Mratibu wa Damu Salama mkoani Shinyanga, Dkt. Joeli Mdale akimhudumia Askofu Josephat Msila kutoka kanisa la Kipentecoste (TMRC) Ndembezi mjini Shinyanga wakati akichangia damu. Zoezi la uchangiaji damu salama likiendelea. Askofu Josephat Masaga kutoka kanisa la (TAG) Shinyanga akiombea amani mkoani Shinyanga katika kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu 2019. 

No comments:

Powered by Blogger.