LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mongella aagiza upanuzi Kituo cha Afya Bwisya ukamilike

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ameagiza ujenzi na upanuzi wa Kituo cha Afya Bwisya kilichopo katika Kisiwa kidogo cha Ukara wilayani Ukereni kukamilika ifikapo Juni 17, 2019.

Mongella alitoa kauli hiyo jana Ijumaa Juni 07, 2019 baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya Kituo hicho kinachoboreshwa kwa hadhi ya Hospitali ikiwa ni maelekezo ya Rais Dkt. John Magufuli baada ya ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere mwaka jana.

Itakumbukwa Novemba 17, 2018 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo alizindua shughuli hiyo inayofanywa na kampuni ya SUMA JKT kupitia usimamizi wa Kamati Maalum iliyoundwa na RC Mongella.
Na George Binagi-GB Pazz, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa pili kulia) pamoja na viongozi mbalimbali akikagua ramani ya upanuzi wa Kituo cha Afya Bwisya.
Kituo cha Afya Bwisya kikikamilika na kuanza kutoa huduma za afya, kitaondoa adha kwa zaidi ya wakazi 30,000 wa Kisiwa cha Ukara waliokuwa wakivuka maji ndani ya Ziwa Victoria kufuata huduma katika Kisiwa cha Nansio mjini Ukerewe ama jijini Mwanza.
Sehemu ya majengo mapya katika Kituo cha Afya Bwisya kisiwani Ukara.
Zaidi ya shilingi Milioni 800 zimetengwa kukamilisha shughuli hiyo ikiwa ni sehemu ya fedha zilizotokana na rambirambi kufuatia ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere kilichokuwa kinatokea Kisiwa cha Bugolora kwenda Kisiwa cha Ukara.
Nyumba mbili za watumishi zenye uwezo wa kuchukua familia/ watumishi mbili zimejengwa.
Nyumba mpya (Two in One) katika Kituo cha Afya Bwisya.
Takribani majengo manane mapya yamejengwa katika Kituo cha Afya Bwisya na hivyo kuwa na hadhi ya kutoa huduma za afya kwa ngazi ya Hospitali.
Baadae Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alikagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa madarasa na maabara katika Shule ya Sekondari Nyamanga iliyopo Kisiwani Ukara. Ujenzi wa Shule hii ulikuwa umesuasua tangu mwaka 2014 licha ya baadhi ya madarasa kukamilika.
Baada ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari Nyamanga Mei 02, 2019 tayari wanafunzi wa kidato cha kwanza wamehamishiwa kwenye shuleni hapo na hivyo kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu hadi Kata jirani.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.