Header Ads

Wajasiriamali wachangamkia fursa Maonesho ya Nane Nane 2019

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Wafanyabiashara wadogo, wakati na wakubwa wamechangamkia maonesho ya wakulima, wafugaji na wavuvu maarufu kama Nane Nane, ambayo kwa Kanda ya Ziwa Magharibi yanafanyika katika uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza.

Kamera ya BMG imenasa matukio kadhaa hususani ya wafanyabiashara wadogo (wajasiriamali) wakitumia uwepo wa maonesho hayo kuuza bidhaa zao kwa wananchi ambao tayari wameanza kujitokeza kwa wingi.

Maonesho ya Nane Nane yaliyoanza Agosti 01, 2019 yanafanyika katika Kanda mbalimbali nchini ambapo Kanda ya Ziwa Magharibi inayohusisha mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera uzinduzi rasmi unafanyika leo Agosti 03, 2019 huku kitaifa yakifanyika katika uwanja wa Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu.

Kwa wanaohitaji huduma ya kutangaziwa Mubashara (LIVE) bidhaa zao/ mabanda yao kwenye maonesho ya Nane Nane Kanda ya Ziwa Magharibi wanahimizwa kuwasiliana na BMG Online TV kupitia nambari 0757 43 26 94.
#BMGHabari
 Mmoja wa wafanyabiashara wadogo akiendelea na shughuli zake katika maonesho ya Nane Nane 2019 uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza.
 Mfanyabiashara mdogo akiendelea na biashara zake katika uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza.
 Wateja wakiendelea kujipatia mahitaji yao kwa mmoja wa wafanyabiashara katika maonesho ya Nane Nane 2019 uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza.
 Bidhaa mbalimbali zinapatikana kwenye maonesho hayo.
 Mashirika, makampuni na taasisi mbalimbali zinashiriki maonesho hayo.
 Mwonekano wa jukwaa kuu kuelekea ufunguzi rasmi wa maonesho ya Nane Nane 2019 Kanda ya Ziwa Magharibi leo Agosti 03, 2019.
 Taswira kuelekea ufunguzi rasmi wa Nane Nane Kanda ya Ziwa Magharibi.
 Wananchi wanaendelea kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho hayo.

No comments:

Powered by Blogger.