LIVE STREAM ADS

Header Ads

TMA yawapiga msasa wanahabari kuhusu mwelekeo wa mvua za vuli

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imefanya warsha na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini kuhusiana na mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba 2019. 

Warsha hiyo ilifanyika Septemba 02, 2019 ikiwa ni mwendelezo wa juhudi za TMA kuhakikisha taarifa zake hasa za utabiri wa hali ya hewa zinawafikia walengwa ikiwemo jamii kwa uhakika na usahihi zaidi.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi alisema taarifa za hali ya hewa zikiifikia jamii kwa haraka, uhakika na usahihi zinasaidia jamii kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa na pia zinasaidia mamlaka zinazohusika kupanga mipango ya kukabiliana na majanga yatokanayo na hali mbaya ya hewa, upatikanaji wa chakula na lishe bora pamoja na afya kwa ustawi wa jamii.

"Kama mnavyofahamu Serikali ya awamu hii ya tano inatambua vyema mchango mkubwa wa huduma za hali ya hewa nchini na umuhimu wa kuwafikia wananchi wote kwa wakati. Hivyo basi ili kudhihirisha hilo Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imekuwa ikihakikisha inakutana na wanahabari ambao ni daraja muhimu kati ya taasisi zetu za serikali na wananchi wote kwa ujumla na kuwaelimisha zaidi" alisema Dkt. Kijazi.

Alibainisha kuwa lengo kuu la warsha hiyo ilikuwa kujadili mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba 2019 na athari zinazoweza kujitokeza. Katika warsha hiyo wataalamu wa TMA waliwasilisha rasimu ya mwelekeo huo na viashiria vilivyopelekea kupatikana kwa utabiri mpya wa mwezi Oktoba hadi Disemba 2019 na kujadili pamoja na wanahabari kabla ya kupata uelewa wa pamoja na kurahisisha uwasilishwaji wake kwa jamii katika lugha inayoeleweka.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi akizungumza kwenye warsha hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dkt. Hamza Kabelwa.
Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa akifafanua jambo kwenye warsha hiyo.
Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri - TMA, Samwel Mbuya (kushoto) akifafanua jambo katika warsha hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu TMA, Dkt. Agnes Kijazi.
Mmoja wa wataalam kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (kulia) akiwasilisha mada kwenye warsha hiyo.
Afisa Uhusiano wa TMA, Monica Mutoni (kushoto) akifafanua jambo katika warsha hiyo.
Washiriki wakifuatilia warsha hiyo.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi (wa tatu waliokaa) baada ya kufunga warsha hiyo.
Na Joachim Mushi

No comments:

Powered by Blogger.