Maonesho ya taasisi za fedha Mwanza "wakulima wahimizwa kujiunga na TAHA"
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa
Mwanza, John Mongella amewahimiza wakulima wa mbogamboga na matunda kujiunga na
kujiunga na taasisi ya TAHA (Tanzania Horticultural Association) ili kunufaika
na fursa mbalimbali zinazopatikana kupitia taasisi hiyo ikiwemo dhamana za mitaji
na masoko.
Mongella
ametoa rai hiyo wakati akifungua Maonesho ya Taasisi za Fedha kuhusu fursa za
upatikanaji wa mitaji kwenye sekta ya Kilimo yanayofanyika kwa siku mbili
kuanzia Novemba 15, 2019 katika eneo la Rock City Mall.
Maonesho
hayo yameandaliwa na taasisi ya TAHA yakiwa na kaulimbiu isemayo “upatikanaji
wa mitaji ya uhakika kwa ukuaji wa kilimo biashara kuelekea uchumi wa viwanda”
inayolenga kuchochea upatikanaji wa mitaji kwa wakulima kupitia taasisi za
kifedha.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye ufunguzi wa maonesho hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya TAHA, Peter Gongoseke akitoa salamu zake kwenye ufunguzi wa maonesho hayo.
Mkurugenzi Mtendaji TAHA, Jacqueline Mkindi akitoa ufafanuzi kuhusiana na maonesho hayo.
Afisa Mahusiano Kitengo cha Biashara kutoka StanBank, Samson Maduka akitoa salamu za benki hiyo ambayo ni mdhamini wa maonesho hayo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akipata maelezo baada ya kutembelea banda la TAHA kwenye maonesho hayo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akikagua mabanda mbalimbali.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini
No comments: