LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais FEMATA "fedha za Uchaguzi 2020 tununulie vifaa vya uchimbaji"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), John Bina ametoa maoni yake binafsi akisema hakuna sababu ya kufanyika Uchaguzi Mkuu 2020 na badala yake fedha zilizotengwa kwa ajili ya Uchaguzi huo zitolewe kwa wachimbaji madini ili wanunulie zana za uchimbaji.

Bina aliyasema hayo Disemba 27, 2019 wakati akitoa salamu kwenye hafla ya ufunguzi wa soko kuu la madini Wilaya Chato lililopo eneo la Buseresere mkoani Geita na kuongeza kuwa watanzania wameridhishwa na kazi kubwa inayofanywa na Serikali chini ya Rais Dkt. John Magufuli hivyo hawaoni sababu ya kuwepo uchaguzi huo.
#BMGHabari
 Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza na wachimbaji wa madini, madalali pamoja na wananchi kabla ya kufungua rasmi soko la madini Chato.
 Katibu Tawala Mkoa Geita, Denis Bandisa akitoa salamu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel.
 Mkuu wa Wilaya Chato, Mhandisi Charles Kabeho akitoa salamu zake kwenye hafla hiyo.
Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akitoa salamu zake kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa soko la madini Wilaya Chato ambapo alisema mazingira kwa wachimbaji wadogo yataendelea kuboreshwa ikiwemo kufikisha umeme katika maeneo yao ya uzalishaji.
Tazama BMT TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.