LIVE STREAM ADS

Header Ads

Daraja la Mto Simiyu lafungwa kupisha matengenezo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Serikali imesitisha matumizi ya daraja la Mto Simiyu lililopo Wilaya ya Magu mkoani Mwanza kwa muda wa siku 10 kuanzia Jumapili Machi 08, 2020 ili kupisha matengenezo ya daraja hilo ambalo limeundwa kwa vyuma.

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amesema katika kipindi hicho cha siku 10, matumizi ya daraja hilo linalounganisha mikoa ya Mwanza, Simiyu, Mara na nchi jirani ya Kenya yatakuwa yanasitishwa kuanzia majira ya saa tatu kamili usiku hadi saa kumi na moja alfajiri.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.