LIVE STREAM ADS

Header Ads

Misungwi watoa zawadi za vinyago kwa Shule zilizofanya vibaya

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Halmashauri ya Wilaya Misungwi mkoani Mwanza imeanza imetoa zawadi za vinyago kwa viongozi wa Kata zilizopata ufaulu wa daraja sifuri katika matokeo ya mitihani ya Taifa kwa Shule za Msingi na Sekondari kwa mwaka 2019 hatua itakayoibua ushindani na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.

Katika matokeo hayo, Kata ya Nhundulu ilishika nafasi ya mwisho kiwilaya huku Shule ya Sekondari Mawematatu iliyopo Kata ya Mabuki pamoja na Shule ya Msingi Mwamazengo iliyopo Kata ya Lubili zikishika mkia kiwilaya na kuibuka na zawadi za vinyago.

Shule za Msingi zilizofanya vizuri na kuibuka na zawadi za ni Shule binafsi ya Lwasa English Medium pamoja na Shule tatu za Serikali ambazo ni Mwakiyenze, Kwimwa na Ngeleka.

Kwa upande wa Sekondari, Shule zilizofanya vizuri ni Shule binafsi ya Ipwaga Sekondari pamoja na Shule ya Serikali Mbarika ambazo zimefuta daraja sifuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana.

Wakati matokeo hayo yakiashiria kiwango cha juu cha ufaulu wilayani Misungwi, Shule tatu za Serikali kati ya Shule 28 za Sekondari za Wilaya hiyo zimeibuka Shule bora katika matokeo hayo.

Zawadi zilizotolewa kwa Shule bora za Sekondari ni vifaa vya maabara pamoja na fedha taslimu shilingi milioni tatu, wakati Shule za Msingi zikipatiwa fedha taslimu shilingi milioni moja na laki nne.

Pamoja na ushindi huo pia shule ya Sekondari Misungwi imeibuka kidedea baada ya kufuta daraja la nne na daraja sifuri katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha sita mwaka jana.

Shule nyingine zilizofanya vizuri wilayani Misungwi ni pamoja na Mbalika Sekondari, Nyabumhanda Sekondari pamoja na Sekondari ya Paulo Bomani ambazo wahitimu wake wamefaulu kwa daraja la daraja la kwanza, pili na la tatu.

Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza inajumla ya Shule za Msingi 149 ambapo kati hizo Shule tisa zinamilikiwa na watu binafsi huku Shule za Sekondari zikiwa 34 ambapo kati ya hizo Shule sita zinamilikiwa na watu binafsi.

No comments:

Powered by Blogger.