Maendeleo ya Ujenzi wa Soko la Kisasa Mirongo jijini Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Baada ya
kufanya utafiti na kubaini wafanyabiashara wadogo hususani wanawake
wanakabiliwa na mazingira magumu ya kufanyia biashara, shirika la kutetea haki
za wanawake na wasichana (KIVULINI) limesaidia upatikanaji wa fedha kwa ajili
ya uboreshaji wa soko la Kiloleli lililopo Wilaya Ilemela pamoja na Mirongo
katika Wilaya ya Nyamagana.
Uboreshaji
wa masoko hayo unahusisha ujenzi na ukarabati wa miundombinu bora na rafiki
kibiashara ikiwemo vyoo, mitaro ya kuzuia maji kuingia sokoni, eneo maalumu kwa
watoto kuchezea na akina mama kunyonyeshea pamoja na Kituo cha daladala
Kiloleli.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Soko la
Kiloleli linatarajiwa kugharimu shilingi Milioni 127 ikiwa ni pamoja na
miundombinu iliyotajwa hapo juu huku soko la Mirongo likigharimu shilingi
Milioni 90.8 ambapo ujenzi huo unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi
mitatu kuanzia mwezi Februari 2020.
Ungana na
BMG TV kujua hatua ulipofikia ujenzi wa soko la Mirongo.
No comments: