LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAT wakabidhi Barakoa mkoani Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kimekabidhi barakoa zipatazo elfu nne kwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella kwa ajili ya kuzigawa katika maeneo mbalimbali ili kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya Corona (Covid- 19).

Mwakilishi wa Chama hicho mkoani Mwanza, Dkt. Rebecca Samwel amesema hatua hiyo inatokana na uhitaji mkubwa wa barakoa uliopo hususani katika maeneo ya kutolea huduma za afya hivyo ni vyema wadau wengine wakajitokeza kuunga mkono jitihada hizo.

Akipokea barakoa hizo, Mongella ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuzingatia taratibu zinazotolewa na Serikali katika kupambana na maambukizi ya Corona ikiwemo matumizi sahihi ya barakoa, kutakasa ama kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia maji tiririka na sabuni.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella (kulia) akiwa na Mganga Mkuu Mkoa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa (kushoto) kupokea barakoa kutoka kwa Mwakilishi wa MAT Dkt. Rebecca Samwel (katikati).

No comments:

Powered by Blogger.