LIVE STREAM ADS

Header Ads

Musukuma azua balaa “apewa onyo kali”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Mwenyekiti wa Kamati inayosimamia zoezi la upuliziaji wa dawa ya kuangamiza virusi vya Corona kwenye vyombo vya usafiri mkoani Mwanza, Yusuph Lupilya amemuonya mbunge wa Geita Joseph Kasheku “Musukuma” ambaye pia ni mdau wa usafirishaji kuacha mara moja kupotosha umma juu ya zoezi hilo alilodai linatekelezwa bila kufuata utaratibu.

Lupilya ametoa onyo hilo Jumamosi Aprili 11, 2020 wakati akiendelea kusimamia zoezi la upuliziaji dawa hiyo kwenye vyombo vya usafiri katika vituo mbalimbali jijini Mwanza ikiwa ni siku moja tu baada ya Musukuma kugomea zoezi hilo.
#BMGHabari
 Timu ya upuliziaji dawa ya kuangamiza virusi vya Corona katika vyombo vya usafiri mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa afua za kupambana na maambukizi ya virusi hivyo.
 Zoezi la upuliziaji dawa ya kuangamiza maambukizi ya virusi vya Corona katika vyombo vya usafiri mkoani Mwanza ikiwa ni tahadhari ya kupambana na maambukizi ya virusi hivyo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.