LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwanza “Viongozi wa Dini na Serikali waungana kuliombea Taifa”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Viongozi wa Makanisa na Serikali mkoani Mwanza wameungana na kufanya maombi ya pamoja katika Kanisa la AIC Makongoro kwa lengo la kuliombea Taifa ili kuondokana na janga la maambukizi ya virusi vya Corona (Covid- 19). 

Maombi hayo yalifanyika Jumamosi Aprili 18, 2020 huku yakizingatia mwongozo uliotolewa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kila mwananchi kwa imani yake kushiriki maombi ya siku tatu mfululizo kuanzia Ijumaa Aprili 17, 2020 ili kumuomba Mwenyezi Mungu kulinusuru Taifa na janga hilo la Corona.
#BMGHabari
Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella, Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dkt. Philis Nyimbi pamoja na Mkuu wa Wilaya Ilemela Dkt. Severine Lalika ni miongoni mwa viongozi wa Serikali mkoani Mwanza waliohudhuria maombi hayo yaliyofanyika Jumamosi Aprili 18, 2020.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.