LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wakala auza sukari kwa bei 'chee' mikoa ya Kanda ya Ziwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
TFDA yaonya matumizi ya sukari ya kijiko kimoja - Mwananchi
Na Charz Mset, Mwanza
Wakala na msambazaji mkubwa wa sukari katika mikoa ya Kanda ya Ziwa VH. Shah ameendelea kuuza sukari katika mikoa hiyo kwa bei elekezi inayotakiwa na Serikali.

Hivi karibuni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa aliwaonya baadhi ya mawakala "wapigaji" wa sukari nchini kuacha kupandisha bei kwa madai ya kwamba bidhaa hiyo imeadimika nchini huku akisisitiza kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kwa atakaebainika.

Msimamo huo wa SHAH ni njia moja wapo ya utekelezaji wa agizo la Serikali la kuwataka wasambazaji (mawakala) wa sukari nchini kuuza sukari kwa mjibu wa taratibu.

Akizungumza Aprili 17, 2020 alisema sukari yote iliyopo katika magahara yake inatauzwa kwa watu wote bila kubagua mtu au mfanyabiashara yeyote yule.

Pia alisema bei ya sukari inayouzwa (na wao) ni bei ya chini ya bei elekezi iliyoelekezwa na Serikali huku akisisitiza kuwa hakuna sababu ya wao kupandisha bei.

"Sisi tunauza sukari mpaka chini ya bei elekezi, lakini unaweza kushangaa leo tumeuza sukari ya kilo 50 kwa Tsh. 130,000 lakini kesho ukakuta tumeuza chini hapo.

"V.H.Shah hatujawahi kupandisha bei na tunafanya kazi kwa mjibu wa sheria hatuwezi kufanya kosa la kupandisha bei ya sukari, tunafahamu tukipandisha bei ni kosa na tunaweza kufutiwa hata leseni na tunafanya kazi hii kwa kusasaidia wananchi wetu " alisema Shah.

Alisema kazi ya kusambaza sukari kanda ya ziwa wanaifanya kwa kufuata sheria na kanuni za biashara za nchi pamoja na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli anaepambana kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa kati.

"Rais wetu Magufuli anafanya kazi ya kuhakikisha nchi hii inakuwa na uchumi kupitia viwanda, sasa sisi tunafanya kazi hii ili kusaidiana nae, lakini unakuta kuna watu wanaongea mambo ya kwamba sisi tumepandisha bei kitu ambacho sio kweli" alisisitiza.

Pia aliwaondoa wasiwasi wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa na kuwahakikisha kuwa sukari ipo ya kutosha na hakuna bei iliyopandishwa ya uuzwaji wa sukari.

Mkoa wa Mwanza, sukari ya KG 50 inauzwa kwa Tsh. 130,000 huku mfuko wa KG 25 ukiuzwa kwa Tsh. 60,000 ambapo hiyo ni bei ya jumla.

No comments:

Powered by Blogger.