LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la Plan International lasaidia mapambano dhidi ya Corona

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Shirika la Plan International limeendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona kwa kukabidhi msaada wa barakoa zaidi ya elfu 10 pamoja na chupa za kugawia vitakasa mikono katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza. 

Akipokea msaada huo Alhamisi Mei 14, 2020 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella aliwahimiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona ikiwemo kuvaa barakoa, kupiga nyungu na kufanya mazoezi huku shughuli za uzalishaji zikiendelea kama Serikali ilivyoelekeza.
#BMGHabari
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (katikati) akipokea barakoa kutoka kwa Meneja Miradi wa shirika la Plan International Mkoa Mwanza, Majani Rwambali (kulia). Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.