LIVE STREAM ADS

Header Ads

UVCCM Iringa wakabidhi vifanyaa vya kujikinga na Corona

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Iringa, Makala Mapesah akizungumzia msaada wa ndoo maalum za kusaidia kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona uliotolewa na jumuiya hiyo.
Na Fredy Mgunda, Iringa
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Iringa vijijini umeeleza kuwa zoezi la uelimishaji jamii pamoja na ugawaji wa vifaa kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya corona ni zoezi endelevu wanalolitekeleza kwa sasa ili kuiepusha jamii na maambuzi.

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Iringa, Makala Mapesah alisema kuwa tangu ilipogindulika kuwapo kwa maambukizi ya Virusi vya Corona nchini UVCCM walianzisha mkakati maalum wa uelimishaji jamii katika vijiji vyote vya wilayani humo sambamba na ugawaji wa vifaa ikiwemo ndoo za maji na sabuni ili kuwawezesha kutajitakasa kama inavyoelekezwa na wataalam wa afya.

Makala alisema kuwa kando ya kuifikia jamii moja kwa moja kwa namna salama ya kujikinga na maambukizi pia wamekuwa wakitumia vyombo vya habari ikiwemo Radio,Runinga, vipeperushi, magazeti na mitandao ya kijamii kwa lengo la kuhakikisha kila mmoja anafikiwa na elimu sahihi na kuepuka maambikizi vya virusi vya Corona vinavysababisha ugonjwa wa Covid 19.

Alisema kuwa wamefanikiwa kutoa msaada wa ndoo maalum za kutakasia mikono,vitakasa mikono na Barakola kwa wananchi katika vijiji vyote ili waendeleee kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo vinavyohatarisha maisha ya binadamu duniani kote.

“Tumefanikiwa kutoa elimu hii kwa ushirikiano wa ofisi za serikali,viongozi wa chama cha Mapinduzi mkoa na wilaya ya Iringa,wabunge na wadau mbalimbali ambao walifanikisha kuwafikia wananchi kwa kutoa elimu na misaada mbalimbali ya kujikinga na kupambana na virusi vya Corona” alisema Makala.

Aliwaomba wadau na viongozi mbalimbali kuendelea kutoa elimu ya kupambana na virusi vya Corona hasa vijijini kwa kuwa bado hawana elimu ya kutosha juu ya vurusi hivyo pamoja changamoto ya kupatikana kwa Barakola limekuwa tatizo kwa wananchi hasa wa maeneo hayo.

Aidha Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Iringa Makala Mapesah sambamba na hayo alizungumzia kuhusu changamoto inayowakabili wakazi wa kijiji cha Isele kitongoji cha Mbingama waliokumbwa na mafuriko katika mvua za msimu huu na kueleza kuwa wanaendelea kuwafikishia misaada ya hali na mali ikiwemo inayotolewa na wadau wa chama cha mapinduzi wakiwemo viongozi wa chama hicho tawala nchini.

Alisema Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya iringa walifanikiwa kuwatafutia Chakula,Nguo,Makazi na pamoja na baadhi ya vifaa tiba ili kuongeza hamasa kwa wataalam wa afya kuendelea kuwahudumia kwa ufanisi wananchi hao kwa kushirikiana na serikali ya Wilaya ya Iringa.

“Tunapenda kumshukuru mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela na viongozi wake kwa kuwatafutia makazi mapya wananchi waliokuwa wamekubwa na mafuriko katika kitongoji cha Mbingama” alisema Makala.

Makala katika hatua nyingine aliipongeza kampuni ya QWIHAYA kwa msaada walioutoa kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko katika Kijitongoji cha Mbingama kijiji cha Isele tarafa ya Pawaga na kuongeza kuwa kampuni hiyo imekuwa mdau mkubwa hasa kwenye utatuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi katika kipindi cha majanga, mbalimbali ikiwemo mafuriko na janga hili la sasa la maambukizi ya corona nchini.

“Kampuni ya QWIHAYA imesaidia sana hata kwenye kujikinga na maambukizi ya kupambana na virusi vya Corona kwa kutoa msaada wa vifaa vya kijikinga na virusi hivyo mkoani Iringa na Tanzania kwa ujumla” Alisema Makala.

Mwenyekiti huyo wa UVCCM Wilayani Iringa Mkala Mapesah alizihimiza kampuni zingine za mkoani Iringa na Nje ya Iringa pamoja na wadau wa maendeleo kwa ujumla kuiga mfano wa Kampuni ya QWIHAYA kwa kuendela kushirikiana na Serikali ya chama cha Mapinduzi katika kusaidia utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii katika kipindi hiki cha maambukizi ya virusi vya corona.

No comments:

Powered by Blogger.