LIVE STREAM ADS

Header Ads

Afisa Shirika la KIVULINI akamatwa akikabidhi msaada Tarime

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Afisa Miradi wa Shirika la KIVULINI pamoja na Mwanaharakati wa kujitolea ngazi ya jamii, Nashon Marwa wamekamatwa na jeshi la polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya Tarime muda mfupi baada ya zoezi la kukabidhi pikipiki kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia wilayani humo.

Mkuu wa Wilaya Tarime, Mtemi Msafiri amesema amechukua hatua hiyo baada ya shirika hilo kushindwa kuwasilisha kwake taarifa ya utendaji wake wa kazi katika Wilaya hiyo kama alivyoagiza hapo awali.
#BMGHabari
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally amesema taratibu zote za kukabidhi pikipiki hizo zilifuatwa hivyo maamuzi ya Mkuu huyo wa Wilaya huenda yalitokana na mkanganyiko wa mawasiliano kuhusu taarifa alizohitaji.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya Tarime, Ocheng' Wayoga (kushoto) akikata utepe kuashiria mapokezi ya pikipiki hizo. Wanaoshuhudia ni maafisa wa polisi Wilaya Tarime akiwemo Mkuu wa Polisi wilayani humo (katikati).
Pikipiki hizo zitasaidia kufuatilia matukio ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake wilayani Tarime ikiwemo ukeketaji, mimba na ndoa za utotoni.
Viongozi na watendaji mbalimbali wilayani Tarime wakipokea pikipiki kutoka shirika la KIVULINI.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.