LIVE STREAM ADS

Header Ads

Taasisi ya TGNP Mtandao yawapiga msasa Waandishi wa Habari

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wandishi wa Habari Tanzania wametakiwa kuandika habari ambazo zitasaidia kuelimisha wanawake na vijana namna ambavyo wanapaswa kushiriki katika shughuli mbalimbali katika jamii ikiwemo kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.

Hayo yamebainishwa na Mwezeshaji Ananilea Nkya kutoka mtandao wa kijinsia Tanzania TGNP wakati wa kuwajengea uelewa na uwezo waandishi wa habari namna ambavyo wanapaswa kuandika na kuleta mwamko kwa kundi la wanawake na vijana kushiriki kwenye kinyanganyiro cha uongozi katika jamii.

Aidha Nkya amewataka wanahabari hao kufanya kazi za jamii zaidi ambazo zinagusa na kuibua fikra chanya badala ya kuandika mambo ambayo yanafanywa na viongozi pekee hatua ambayo itatoa mwamko chanya kwa wanawake na vijana ikiwemo kuwania nafasi za uongozi.

Nao baadhi ya waaandishi wa habari kutoka mikoa ya Mara na Shinyanga wamezungumzia namna ambavyo watatumia kalamu zao kuleta mabadiliko katika jamii zinazowazunguka kwa kuhamasisha wanawake kujitokeza zaidi katika masuala ya kisiasa na kuacha kujiona kuwa ni wanyonge.

Aidha wandishi wametakiwa kuongeza kasi ya kuripoti habari za ushiriki wa wanawwke katika uongozi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020.

Dhima ya TGNP Mtandao ni kuondoa uandishi wa zamani ambao umekuwa ukihusisha viongozi pekee na badala yake kuwa na uandishi unaohusisha habari za kijamii zinazowahusisha wanawake na vijana.
Na Asha Shaban, Shinyanga
Mwezeshaji wa mafunzo yaliyoandaliwa na taasisi ya TGNP kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mara na Shinyanga, Ananilea Nkya akiwafafanua jambo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja.

No comments:

Powered by Blogger.