LIVE STREAM ADS

Header Ads

Dkt. Tulia Ackson ataka taasisi yake isihusishwe na masuala ya kisiasa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Taasisi ya Tulia Trust imetoa msaada wa mifuko 140 ya siment katika Shule za Msingi Halinji na Nsalaga zilizopo jijini Mbeya ili kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa unaoendelea katika Shule hizo.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amewataka wananchi kutofautisha misaada inayotolewa na taasisi hiyo na masuala ya kisiasa.

Dkt. Tulia amesema "kuna watu huwa wanachanganya mambo, tuwekane vizuri hapa ili mtu asije kurudi nyumbani akiwa na presha, ndugu zangu muda wa kampeni bado na mimi hapa sijaja kama mgombea bali nimekuja kama kiongozi wa taasisi inayoitwa Tulia Trust" alifafanua Dkt. Ackson.

Aidha Dkt Tulia alisema muda wa kuanza kampeni haujawadia na hadi sasa wagombea bado hawajateuliwa hivyo kila mmoja awe na amani na kutohusisha shughuli za taasisi yake na shughuli za kisiasa.
Na Tonny Alphonce

No comments:

Powered by Blogger.