LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanunuzi wa Pamba watakiwa kuwalipa wakulima kwa wakati

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Makampuni yanayojihusisha na ununuzi wa pamba yametahadharishwa kutokiuka makubaliano ya kufanya malipo kwa wakulima ndani ya masaa 48 baada ya kuchukua pamba kupitia vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS).

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alitoa tahadhari hiyo Jumatano Agosti 12, 2020 wakati akikagua zoezi la ununuzi wa pamba wilayani Magu ambapo ametembelea vyama vya Msingi vya Ushirika Kabila pamoja na Ng’haya.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMGMkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alikagua zoezi la ununuzi wa Pamba katika AMCOS mbalimbali wilayani Magu.Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza na wakulima wa zao la Pamba wilayani Magu ambapo aliwataka wanunuzi kufanya malipo kupitia nambari za simu za wakulima ndani ya masaa 48 baada ya kuchukua pamba katika AMCOS.Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alikagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Wilaya Magu.Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alikagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Wilaya Geita na kuagiza baadhi ya marekebisho kufanyika hususani eneo la vigae (tiles).Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alikagua ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Salamabugatu inayojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya ununuaji pamba ya Alliance Ginneries na kuelekeza Shule hiyo ianze kupokea wanafunzi kuanzia mwezi Septemba 2020.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.