LIVE STREAM ADS

Header Ads

Benki ya CRDB yazindua mikopo ya zana za kilimo kwa wakulima

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Benki ya CRDB kwa kushirikiana na makampuni ya ETC Agro, Lona Agro pamoja na Agricom imezindua rasmi huduma ya mikopo ya zana za kilimo kwa wakulima kwa lengo la kuboresha zaidi shughuli zao na kupata mavuno yenye tija.

Uzinduzi wa huduma hiyo (Agro-Equipment Financing) umefanyika Septemba 23, 2020 nchini nzima kupitia Kanda mbalimbali za Benki hiyo ambapo kwa Kanda ya Ziwa umefanyika katika viunga vya Rock City jijini Mwanza kwa kuwakabidhi wakulima wawili waliojitokeza kukopa trekta na 'power Tira'.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Ilemela, Dkt. Severine Lalika (kulia) akikabidhi mfano wa ufunguo wa trekta kwa bwana Ndim Bunegije (kushoto) ambaye ni mkulima mkoani Mwanza. Anayeshuhudia katikati ni Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Japhary Hassanaly.
Mkuu wa Wilaya Ilemela, Dkt. Severine Lalika (kushoto) akimkabidhi nyaraka mmoja wa wakulima mkoani Mwanza aliyekopa 'power tira' kwa ajili ya kuboresha shughuli zake za kilimo.
Mkuu wa Wilaya Ilemela Dkt. Severine Lalika amewahimiza kuyatumia vyema na kurejesha mikopo yao kwa wakati.
Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Japhary Hassanaly akionesha moja wapo ya aina ya zana za kilimo ambazo wakulima wanaweza kukopa kupitia benki hiyo.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.