MWANZA WAMKOSHA MAGUFULI
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Diamond (WCB) wakitumbuiza.

Wakazi wa Mkoa Mwanza wamekosha mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli kwa jinsi walivyojitokeza kwa wingi kumsikiliza kwenye uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 mkoani Mwanza uliofanyika Jumatatu Septemba 07, 2020 katika uwanja wa CCM Kirumba.
Akiomba kura kwa wananchi ili kumchagua kuwa Rais wa Tanzania kwa awamu ya pili inayoanza mwaka 2020/25, Dkt. Magufuli amesema hatawaangusha na atatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ile aliyoianza katika awamu ya kwanza 2015/20.
Ameomba kura za kutosha kwa wagombea wa CCM siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, 2020.
Mgombea urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu mkoani Mwanza.
Mgombea ubunge Jimbo la Nyamagana kupitia CCM, Stanslaus Mabula akiomba kura kwa wananchi baada ya kupewa nafasi hiyo na mgombea urais Dkt. John Pombe Magufuli.Wagombea udiwani CCM mkoani Mwanza wakitambulishwa kwa wananchi.
Mgombea urais, Dkt. John Pombe Magufuli akiwaombea kura wagombea udiwani na ubunge mkoani Mwanza.Viongozi mbalimbali wakiwemo wa vyama vya siasa, Serikali na dini wamehudhuria mkutano huo.Diamond (WCB) wakitumbuiza.
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Hamfrey Polepole akifanya utambulisho na kuongoza itifaki katika mkutano huo.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini
SOMA>>> Mapokezi ya JPM Mwanza
No comments: