LIVE STREAM ADS

Header Ads

TCRA yazionya 'Cable TV' kwa kurusha Chaneli za kulipia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewaonya warusha matangazo ya runinga kwa njia ya waya 'Cable TV' kurusha matangazo mbalimbali ikiwemo mpira pamoja na tamthilia kutoka kwenye chaneli za kulipia bila kuwa na kibali kutoka kwa wamiliki wa chaneli hizo.

Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandinsi Francis Mihayo alitoa onyo hilo Januari 13, 2021 kwenye kikao baina ya mamlaka hiyo na wamiliki wa 'Cable TV' na wadau wengine ikiwemo shirikisho la soka Tanzania (TFF) pamoja na warusha matangazo kupitia visimbuzi vya kulipia.

Mhandisi Mihayo alisema watoa huduma za matangazo kwa njia ya waya 'Cable TV" hawaruhusiwi kurusha matangazo kutoka kwenye chaneli za kulipia bila kuwa na kibali kutoka kwa makampuni yaliyopewa haki miliki ya matangazo hayo kama vile Azam Media, Multchoice/ DSTV, Zuku, Star Times.

Alibainisha kuwa hapo awali kulikuwa na ukiukwaji wa sheria kwa 'Cable TV' kurusha matangazo kutoka kwenye chaneli za kulipia (Pay TV) ambapo ni kinyume pia na leseni yao inayowataka kurusha matangazo kutoka kwenye chaneli za bure (Free to Air) hivyo kikao hicho kitasaidia watoa huduma hao kufanya kazi kwa kufuata sheria ya haki miliki ya mwaka 1999 na kanuni zake.

Nao baadhi ya warusha matangazo kwa njia ya waya 'Cable TV' walilalamikia adha wanayoipata kwa kurusha chaneli za bure kutoka nje ya nchi na kushauri TCRA kuondoa mkanganyiko huo kwani leseni yao inawaruhusu kurusha chaneli za bure ambapo wamekuwa wakiitwa majina yasiyofaa 'maharamia' wakati wanafanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandinsi Francis Mihayo (katikati) akizungumza kwenye kikao hicho kilichofanyika jijini Mwanza kikiwashirikisha warusha matangazo kwa njia ya waya 'Cable TV' kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Wadau mbalimbali wakifuatilia kikao hicho.
Watoa huduma za utangazaji kwa njia ya waya 'Cable TV' walilalamikia oparesheni ambazo zimekuwa zikifanywa na makampuni yenye haki miliki za kurusha matangazo ya mpira na kushauri TCRA kuhakikisha oparesheni hizo zinafanywa kwa kufuata sheria.
Watoa huduma ya utangazaji kwa njia ya waya wakifuatilia kikao hicho.
Tazama BMG TV ahapa chini

No comments:

Powered by Blogger.