LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kamati ya Ushauri yaridhishwa na usimamizi wa miradi Nyamagana

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mwonekano wa jengo la wodi ya wanaume katika Hospitali ya Wilaya Nyamagana, Butimba mkoani Mwanza ambayo imegharimu shilingi bilioni 1.4 hadi kukamilika kwake.

Wajumbe wa Kamati ya Ushauri (DCC) Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wametembelea miradi mbalimbali ya maendeleo na kuridhishwa na utekelezaje wake huku wakiwapongeza Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dkt Phili Nyimbi pamoja na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba kwa kusimamia vyema miradi hiyo.

Miradi waliyotembelea wajumbe hao ni pamoja na ujenzi wa soko kuu Mwanza, stendi ya mabasi Nyegezi, wodi ya wanaume hospiyali ya Butimba, dampo la kisasa Buhongwa pamoja na miundombinu katika Shule ya Msingi Iseni B pamoja na Shule ya Sekondari Buhongwa.

Baada ya ziara hiyo, wakasema ikitokea Rais Dkt. John Pombe Magufuli anataka kuwahamisha viongozi hao katika Wilaya ya Nyamagana watamuomba awaache kwanza ili wakamilishe utekelezaji wa miradi hiyo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wajumbe wa Kamati ya Ushauri (DCC) Wilaya ya Nyamagana pia walikagua ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa katika Shule ya Msingi Iseni B ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa mwaka 2019 aliposimama katika Kata ya Butimba na mmoja wa wanafunzi wa Shule hiyo akaomba wanafunzi wajengewe madarasa.
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza akifuatilia mpangilio wa vyumba vya madaraa katika Shule ya Msingi Iseni B.
Wajumbe wa Kamati ya Ushauri (DCC) Wilaya ya Nyamagana pia walikagua ujenzi wa jengo la abiria na uwekezaji linalojengwa katika eneo la stendi mpya ya Nyegezi ambapo hadi kukamilika litagharimu shilingi bilioni 15.885.
Mkandarasi anayejenga stendi hiyo ni kampuni ya Mohamed Builder.
Wajumbe wa Kamati ya Ushauri (DCC) Wilaya ya Nyamagana walipofika kukagua ujenzi wa jengo la biashara na kusubiria abiria katika stendi ya Nyegezi.
Hatua ulipofikia ujenzi wa jengo hilo ambalo stendi ya kisasa Nyegezi inatarajiwa kukamilika mwaka 2022.
Wajumbe wa Kamati ya Ushauri (DCC) Wilaya ya Nyamagana walishauri mradi huo kukamilika kwa wakati.
Wajumbe wa Kamati ya Ushauri (DCC) Wilaya ya Nyamagana walikagua pia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi B pamoja na Shule ya Sekondari Buhongwa.
Wajumbe wa Kamati ya Ushauri (DCC) Wilaya ya Nyamagana  walikagua ujenzi wa dampo la kisasa Buhongwa ambalo limegharimu shilingi bilioni tisa.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.