LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwenyekiti wa CCM awataka vijana kujitambua 'siyo kubeba mikoba ya wakubwa'

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Nyamagana mkoani Mwanza, Zebedayo Athuman amewataka vijana wa jumuiya ya chama hicho (UVCCM) wilayani humo kujitambua na kutimiza wajibu wao ipasavyo katika kukijenga chama.

Athuman ameyasema hayo Jumamosi Machi 13, 2021 wakati akifungua Mkutano Mkuu Maalum wa UVCCM Wilaya Nyamagana, wenye lengo la kumchagua Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wake Philipo Magori kufariki dunia mwezi Agosti 2020.

Aidha Athumani amesisitiza kuwa kazi ya vijana siyo kubeba 'brifkesi' za wakubwa bali ni kujitambua na kutimiza vyema wajibu wao huku akiwahimiza pia wajumbe wa mkutano huo kutokuwa na mgombea wao mfukoni bali wamchague mgombea mwenye sifa atakayeivusha jumuiya hiyo katika masuala mbalimbali ikiwemo Mkutano wake Mkuu mwakani 2022.

Katika mkutano huo, Katibu wa UVCCM Wilaya Nyamagana, Malanyingi Matukuta amesema jumla ya wagombea 29 walichukua fomu kuwania nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya Nyamagana na waliorejesha fomu walikuwa 25 ambapo waliofanyiwa usaili ngazi ya wilaya na kubaki 23 ambao majina yao yalifanyiwa mchujo ngazi ya Mkoa na kubaki majina matatu ambayo ni Boniphace Zephania, Hassan Hussein na Kisali Simba.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Katibu wa CCM Wilaya Nyamagana, Geofrey Kavenga akitoa salamu kwenye mkutano huo.
Katibu wa UVCCM Wilaya Nyamagana, Malanyingi Matukuta akizungumza kwenye mkutano huo.
Wajumbe wakifuatilia mkutano huo.
Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa, Richard Kashilimu ambaye alikuwa Msimamizi wa uchaguzi huo akitoa mwongozo kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza.
Wajumbe walimchagua Mussa Magana (aliyesimama) Mwenyekiti wa muda wa mkutano huo.
Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya Nyamagana. Kutoka kushoto ni Boniphace Zephania Boniphace, Hassan Hussein Mambosasa na Kisali Simba.
Wajumbe na wageni mbalimbali wakifuatilia mkutano huo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.