LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kalamu za Waandishi wa Habari ni silaha muhimu katika kudumisha Amani

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Ellukagha Kyusa, Mwanza
Siku zote jamii inaamini Sekta ya habari ina nguvu kwenye kuhabarisha umma hasa katika kusisitiza juu ya amani na utulivu katika nchi yoyote duniani.

Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan aLIyasema hayo mbele ya waandishi wa habari wanaopata mafunzo ya kuripoti habari za amani kupitia shirika la International Women Peace Group ( IWPG ).

Aliongeza kuwa waandishi wa habari wana nafasi kubwa katika jamii ya kusambaza habari za amani zinazobeba ujumbe kwa watanzania katika kuendelea kuenzi na kudumisha amani.

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Wabari Mkoa wa Mwanza (MPC), Edwin Soko aliwahimiza waandishi wa habari kutumia fursa hiyo katika kusoma kwa bidii ili wawe mabalozi wazuri kwenye kusisitiza juu ya uwepo wa amani nchini na kukemea vikali uvunjifu wa amani katika jamii kwa kupitia karamu zao.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka IWPG, Thitiwan White alisisitiza waandishi hao kuandika kwa weledi habari za amani ili kuwashawishi watanzania kuitunza na kuiheshimu amani iliyopo nchini kwao.

Zaidi ya waandishi wa habari 15 wamepata fursa ya kuhudhuria mafunzo hayo ambayo yanayoratibiwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC) pamoja na IWPG.

No comments:

Powered by Blogger.