LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waandishi wa Habari Mwanza kuwa mabalozi wa amani

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Edwin Soko, Mwanza
Tanzania ni nchi ya amani, amani iliyopo ni zao kubwa la mwasisi wa Taifa hilo Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mbaye alisisitiza amani tangia Taifa lilipopata uhuru.

Baada ya Nyerere kutoka madarakani marais wengine waliofuta yaani Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Mrisho Kikwete, John Pombe Magufuli na Samia Suluhu wote wamekuwa wakisisitiza amani na upendo kwa watanzania.

Hivi karibuni Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC) kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la International Women Peace Group ( IWPG) liliingia makubaliano ya kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari ya kuandika habari za amani.

Kimsingi mafunzo hayo ni muhimu sana kwa kundi la wanahabari kwa kuwa suala la amani ni muhimu kwa jamii yoyote ile Duniani. MPC na IWPG itaendelea kuwa nguzo muhimu kwenye kutangaza amani Tanzania kupitia waandishi wa habari.

Kujifunza jinsi ya kuandika habari za amani kwa kundi la wanahabari ni jambo la msingi sana nchini Tanzania. Takribani ya waandishi wa habari kumi na tano wanahudhuria mafunzo hayo ya kuandika habari za amani.

Waandishi hao watakuwa mabalozi wazuri wa kuandika habari za amani na kuifanya jamii ijifunze umuhimu wa amani duniani.

Mwakilishi wa IWPG, Thitwan aliwahakimishia waandishi kuwa IWPG itaendelea kufanya kazi bega kwa bega na MPC ili kuwawezesha waandishi hao kumaliza kozi hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.